Searching...
Image and video hosting by TinyPic
5 January 2015
Monday, January 05, 2015

TFF acheni kulala.


Na Oscar Oscar Jr

Chama cha soka nchini Rwanda kimezindua mpango ambao utazingatia umri kwenye mchezo wa soka nchini humo ambapo kwa sasa, ligi daraja la pili itashirikisha vijana ambao wako chini ya miaka 20 na mpango huu utadumu kwa miaka miwili.

Ligi hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa mwezi Januari au mapema mwezi Februari mwaka huu. Akizungumza na Gazeti la Newtimes la nchini Rwanda, Rais wa chama cha soka nchini humo, Vincent de Gaulle Nzamwita amesema kuwa, hii ni fursa kwa vijana na lazima waichangamkie.

Kwa upande wa msemaji wa Shirikisho hilo lijulikanalo kama FERWAFA, Moussa Hakizimana amesema kuwa, ndani ya miaka miwili wanauhakika tayari watakuwa na vijana wengi kwenye soka na hapo ndipo watakaporuhusu ule utaratibu wa hapo awali kurejea ambao hauna ukomo wa umri wa ushiriki.

Pengine huu ndiyo muda wa Tanzania kuweza kuamka na kujifunza kwa wenzetu wa Rwanda badala ya kuendelea kureketeza pesa za watanzania kwa mipango ambayo haitokuja kulikomboa taifa hili kwa upande wa michezo ikiwa ni pamoja na soka. 

Tunahitaji kuona mipango kama hii ikifanywa pia Tanzania mahali ambapo kuna vijana wengi wenye vipaji lakini wanakosa mahali pa kujiendeleza. Hii mipango ya timu ya maboresho ni sawa na kudurudisha kwenye zama za mawe wakati wenzetu wako Dijitali.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!