Na Chikoti Cico
Kiungo wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ivory Coast ambaye kwasasa anaichezea timu ya AS Roma inayoshiriki ligi kuu nchini Italia maarufu kama Seria A Gervinho amevunjiwa nyumba yake iliyopo Axa nchini Italia karibu na mji wa Roma.
Taarifa kutoka La Gazetta Dello Sport zilisema mchezaji huyo aliibiwa baada ya kubandika kwenye ukurasa wake wa tweeter picha akiwahabarisha mashabiki wake 243000 ambao wanamfwatilia kwenye mtandao huo wa jamii kwamba anaelekea nyumbani nchini Ivory Coast.
Taarifa zinasema kwamba watu wasiojulikana walichukua vitu mbalimbali vyenye thamani kubwa kama vito na saa kwenye nyumba hiyo na kaka wa Gervinho ndiye aliyegundua wizi huo na kutoa taarifa kwa kwa polisi.
Gervinho aliyeenda nchini Ivory Coast kwaajili ya mapumziko ya Krismasi anatarajia kurejea nchini Italia siku ya Jumanne.
Gervinho anakuwa mchezaji mwingine wa Roma ambaye ameibiwa baada ya Radja Nainggolan ambaye alikuwa kwenye mapumziko ya Krismasi jijini London kurejea nchini Italia na kukuta gari lake limevunjwa na kupakiwa kwenye kiwanja cha ndege cha Fiumicino huku vioo vikiwa vimeharibiwa na baadhi ya vifurushi kupotea.
0 comments:
Post a Comment