Searching...
Image and video hosting by TinyPic
7 August 2014
Thursday, August 07, 2014

Mbeya City kutwaa ubingwa msimu ujao?


Na Oscar Oscar Jr

Mbeya City pamoja na kumaliza ligi wakiwa nafasi ya tatu, bado ndiyo timu pekee kwenye timu nne bora za juu iliyofunga mabao machache msimu uliopita. 

Safu ya ushambuliaji inayoundwa na Paul Nonga, Saad Kipanga na mtu mzima Mwagane Yeya wote kwa pamoja walifunga mabao 17 tu na kushindwa kufikia hata magoli 19 ya mshambuliaji mmoja wa Simba, Amisi Tambwe.

Kwa kuliona hilo bila shaka ndiyo maana kocha Juma Mwambusi ameamua kumuongeza mshambuliaji Themi Felix kutoka klabu ya Kagera Sugar ambako alifunga mabao tisa msimu uliopita. Yanga walifanikiwa kufunga mabao 61, Azam 51, Simba 41 na Mbeya City waliambualia mabao 32 pekee.

Mbeya City walianza ligi msimu uliopita wakiwa na uoga kitu ambacho kiliwafanya kupata sare michezo mingi ya awali hasa mechi zao za nyumbani na kujikuta wakijikusanyia alama 27 mzunguko wa kwanza. 

Raundi ya pili, waliamua  kujiachia baada ya kuona mazingira ya kutwaa ubingwa yanawezekana na hapo ndipo walipojikuta wanachezea vipigo kutoka kwa Yanga, Coastal Union na Azam. City waliambulia alama 22 pekee mzunguko wa pili na kufanya kuwa na jumla ya alama 49 kwa msimu mzima.

Ili uwe bingwa ni lazima pia uwe na uwezo wa kushinda mechi zako dhidi ya wapinzani wako wa ubingwa kitu ambacho msimu uliopita Mbeya City walishindwa. 

City walipata sare mechi zote mbili dhidi ya Simba, kwenye mechi za Yanga na Azam City walijikuta wakipata sare mechi mbili na kufungwa mechi nyingine mbili na wababe hao. Kwenye michezo sita ya Azam, Simba na Yanga, Mbeya City walipata alama nne tu kati ya 18 walizokuwa wanazigombea.

Mbeya City wanauwezo wa kupigania tena ubingwa msimu ujao ingawa kuna uwezekano mkubwa wachezaji wake wakawa na uchovu kutokana na kutumia nguvu nyingi sana msimu uliopita. 

Pamoja na kuongeza wachezaji wannne (Themi Felix, Peter Mwalianzi, Erick Mawala na Lamboni Asheri) bado wakiweza  kuitete nafasi yao ya tatu msimu ujao itakuwa ni mafanikio kwao na mwenendo mzuri.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!