Ndanda hakuna muda wa kupoteza tena.
Na Oscar Oscar Jr
Baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons kule Jijini Mbeya, timu ya Ndanda leo hii iko safarini kuelekea mkoani Mtwara ambapo weekend hii watashuka dimbani kupambana na timu ya Polis kutoka Mkoani Morogoro.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, kocha mkuu wa timu hiyo, Meja Mstaafu Abdul Mingange amesema wanaelekea Mtwara kuendelea kujifua na kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mchezo unaofuata utakaopigwa Januari 10.
Alipoulizwa kuhusu majeruhi, Mingange amejibu kuwa kuna wachezaji wawili ambao walipata maumivu madogo madogo lakini akasema kuwa hakuna mchezaji atakayeshindwa kucheza kwenye mechi hiyo japo hakutaja majina ya wachezaji hao.
Ndanda sasa wanakamata nafasi ya 11 wakiwa na alama tisa baada ya kuwalaza Tanzania Prisons kwa bao 1-0 kwenye mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Kocha Mingange ameeleza kuwa, timu hiyo itakwenda moja kwa moja kuanza maandalizi na hakuna muda wa kupoteza wakifika Mtwara.
Polis Morogoro ambao ambao wanakamata nafasi ya tano wakiwa na alama 13 watasafiri hadi mkoani Mtwara kuumana na Ndanda Fc na mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu hasa ukizingatia kuwa timu zote hizi zimepanda daraja msimu huu na hivyo hakuna anayemuogopa mwenzie.
0 comments:
Post a Comment