Na Rossa Kabwine
Arsenal wamepeleka dau kwa ajili ya kumsajili beki wa kulia wa klabu ya Juventus, Stephan Lichtsteiner kwenda katika klabu hiyo ya jijini London.
Ripoti kutoka nchini Italia zinasema kuwa kocha wa Arsenal, Arsene wenger anaonekana kumuhitaji sana mchezaji huyo wakimataifa wa Switzerland katika dirisha dogo la usajiri la mwezi Januari.
Arsenal wanaweza kufanikisha dili la kumpata mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kwa sababu, mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni mwa msimu huu ambapo ataondoka kama mchezaji huru.
Mtandao wa Sky Sports umeripoti kuwa, arsenal wapo katika mazungumzo ya juu zaidi na wawakilishi wa Lichtsteiner katika kupata sahihi ya mchezaji huyo amabaye anaweza kucheza nafasi yoyote katika nafasi ya mabeki wanne.
Mchezaji huyo amekuwa akiachwa katika kikosi cha kwanza cha Juventus tangu kocha Massimilliano Allegri kuchukua kibarua cha kuinoa klabu hiyo ingawa kocha huyo anajua uwezo wake wa kupanda na kutengeneza nafasi za magoli
Arsenal na Inter Milan wapo katika mstari wa mbele kuwania sahihi ya mchezaji huyo katika dirisha dogo la Januari ingawa Linchtsteiner anaweza kuongeza mkataba mwingine na timu yake ya Juventus.
Arsenal wanalazimika kuongeza mlinzi mwingine baada ya kumuuza beki wa kati, Thomas Vamerleen kwenda katika klabu ya Barcelona huku majeruhi yanayo waandama Laurent Conscienly na Mathieu Debuchy, yakiacha pengo kwa timu hiyo.
0 comments:
Post a Comment