Na Chiko Cico
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amwomba msamaha mwamuzi wa mchezo wa kombe la FA kati ya Chelsea dhidi ya Watford Kevi Friend baada ya kupinga maamuzi aliyoyafanya kwenye mchezo huo ambao Chelsea walishinda kwa magoli 3-0.
Mourinho akiongea na vyombo vya habari baada ya mchezo huo alionyesha kukerwa na uamuzi wa refa huyo kutoipa Chelsea penati katika tukio ambalo mlinzi wa Watford Craig Cathcart alionekana kuzuia shuti la Diego Costa kwa mkono kabla ya Loic Remy kumalizia mpira huo na kuipa Chelsea goli la pili katika mchezo huo.
Baada ya kujadili tukio hilo Mourinho alimwomba msamaha binafsi lakini pia alimwomba msamaha kupitia vyombo vya habari kwa kusema “ tulikuwa na penati kwa upande wetu lakini niliongea na mwamuzi na nataka niombe msamaha kwa maneno yangu kuhusu yeye mapema kwenye luninga”
“Alichokifanya ni uamuzi mzuri, aliona kwamba ni penati na alikuwa anaitoa lakini aliona kwamba mpira unakwenda kwa Remy na alisubiria kwa sekunde chache, alisema kama Remy asingeweza kuutuliza mpira ama angeupiga juu ya mwamba hakika angetoa penati hivyo nimemwomba msamaha binafsi na namwomba msamaha sasa”
Mourinho ambaye amekuwa akiwalalamikia waamuzi mara kwa mara kwa kufanya maamuzi mabovu dhidi ya Chelsea karibuni alimlalamikia mwamuzi wa mchezo wa Chelsea dhidi ya Totten Ham Hotspur Phil Down kwa kilichoonekana kama kuinyonga Chelsea kwenye mchezo huo ambao Chelsea walifungwa kwa magoli 5-3.
0 comments:
Post a Comment