Searching...
Image and video hosting by TinyPic
5 January 2015
Monday, January 05, 2015

Tetesi za Usajili barani Ulaya.


Na Oscar Oscar Jr

Klabu za Chelsea na Manchester United zimekuwa katika harakati za kupata beki wa kati na kwa mujibu wa magazeti ya leo barani Ulaya, yamemuhusisha beki wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Real Madrid, Rafael Varane kuwindwa na klabu hizo lakini ni lazima klabu inayomtaka Varane iwe tayari kulipa kiasi cha Pauni 20M.

Baada ya kuonekana Liverpool kuwa na tatizo la ushambuliaji licha ya kufunga mabao 26 mpaka sasa kwenye ligi kuu Uingereza, kocha Brendan Rodgers anajiandaa kulipa Pauni 3M kwa klabu ya Lile ili kumrejesha mchezaji wao Divock Origi.

Origi alinunuliwa kipindi cha usajili wa majira ya joto na kumbakiza kwenye klabu hiyo mpaka mwishoni mwa msimu huu. Wanatakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha ili kumrejesha katika kipindi hiki cha January.


Kwa upande wa pili, Manchester City wanamfukuzia kiungo wa kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Schalke 04, Julian Draxle ili kuongeza nguvu wakati Yaya Toure atakapoondoka kwenda kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika lakini klabu hiyo ya Ujerumani haiwezi kumwachia pasipo kulipwa Pauni 25M.

Kiungo Steven Gerrard imedaiwa amekataa ofa ya Pauni 18M kutoka Qatar ambapo amehitajika kwenda kucheza pale mkataba wake na Liverpool utakapo malizika mwishoni mwa msimu huu. Gerrard amekataa ofa hiyo na huenda safari yake ya kuhamia marekani ikatimia.

Kiungo mshambuliaji wa Barcelona, Sergio Busquets huenda akawa amezikacha Arsenal, Chelsea na Manchester United ambazo kwa nyakati tofauti zimekuwa zikimuwani kutokana na mshambuliaji huyo kujiandaa kusaini mkataba mpya na Wakatalunia hao.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!