Mchakato wa kumpata Nahodha mpya wa Liverpool
Na Oscar Oscar Jr
Baada ya taarifa za Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard kutangaza kuondoka Liverpool mwishoni mwa msimu huu na kutimkia kwenye ligi kuu nchini Marekani, kuna kila dalili za kiungo Jordan Hendreson kutangazwa kuwa nahodha mpya wa timu hiyo.
Kocha wa timu hiyo Brendan Rodgers alimtaja Henderson kama Nohodha msaidizi wa timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu na kuondoka kwa Gerrard kuwaweza kumpatia nafasi Jordan ya kuwa Nahodha mkuu.
Akizungumza kuhusu jambo hilo Rodgers amesema kuwa, katika kikosi chake wapo wachezaji wengi ambao wanasifa za kutwaa jukumu hilo na walikuwa na hamu ya kufanya hivyo huku akiwataja Jordan Henderson na Raheem Sterling kama sehemu ya wachezaji wenye uwezo wa kuziba nafasi hiyo ya Uongozi ndani na nje ya uwanja.
Liverpool usiku wa leo watakuwa dimbani kwenye mchezo wa mzunguko wa tatu wa Kombe la FA watakapocheza na AFC Wimbledon ndani ya dimba la Kingsmeadow.
Tayari timu za Arsenal, Chelsea, Manchester United na Manchester City zimeshafuzu kwa mzunguko wa nne wa michuano hiyo iliyoanza kupigwa siku ya Jumamosi.
0 comments:
Post a Comment