Searching...
Image and video hosting by TinyPic
2 December 2014
Tuesday, December 02, 2014

Kun Aguero amfunika Luiz Suarez kwenye tuzo Uingereza.


 Na Chikoti Cico.

Mshambuliaji wa Manchester City na timu ya taifa ya Argentina, Sergio Aguero anyakua tuzo ya mchezaji bora wa mwaka iliyotolewa na shirikisho la mashabiki wa soka (Football Supporters Federation) siku ya Jumatatu katika hafla iliyofanyika kwenye Hoteli ya St Pancras Renaissance jijini London Uingereza.

Aguero ambaye alishinda kombe la ligi ya Uingereza kwa mara ya pili na timu ya Manchester City mapema mwezi wa tano mwaka huu, amechukua tuzo hiyo akimpita mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Luis Suarez ambaye kwasasa anaichezea timu ya Barcelona baada ya kupigiwa kura nyingi na mashabiki.

Katika mwaka 2014 Aguero amefunga jumla ya magoli 16 akipitwa na mshambuliaji wa Swansea Wilifried Bony peke yake, tokea kuanza kwa msimu huu mshambuliaji huyo amefunga jumla ya magoli 17 katika mechi 19 alizocheza.

Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Argentina amenyakua tuzo hiyo huku akiwapita mchezaji mwenzake wa Manchester City Yaya Toure, Raheem Sterling wa Liverpool, Morgan Schneiderlin wa Southampton na wachezaji wa Chelsea, Eden Hazard na Branslav Ivanovic.

Aguero ambaye alipokea tuzo hiyo akiwa na mkewe Karina Tejeda, akionyesha kufurahia tuzo hiyo aliandika kwenye ukurasa wake wa tweeter kwamba;

“ ni tuzo maalum sana kwasababu imetoka kwa mashabiki, shukrani zangu ziende kwao, kwa wachezaji wenzangu na wote kwenye timu ya Manchester City"

Mchezaji huyo aliongeza  "Pia nina furaha kuwepo kati ya wachezaji waliochaguliwa kuwania tuzo ya wachezaji 11 wa FIFA kwa mwaka 2014, imekuwa ni siku ya pekee”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!