Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 December 2014
Thursday, December 04, 2014

Roben Van Persie kuanzia benchi mechi ya Southampton siku ya Jumatatu.


 Na Oscar Oscar Jr

Mshambuliaji wa Manchester United, Roben Van Persie huenda siku si nyingi akaanza kupoteza nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Loius Van Gaal ambaye ameonekana kukubali zaidi mchango wa kijana chipukizi, James Wilson.

Baada ya Nahodha wa timu hiyo Wayne Rooney kuwa nje ya dimba kutokana na kuumia kwenye mchezo wa timu hiyo dhidi ya Hull City, United ilishuhudia ubora wa Wilson 19 ambaye alianza sambamba na Roben Van Persie kama washambuliaji pekee kwenye mechi dhidi ya Stoke City.

Leo taarifa imetoka huku ikibainisha kuwa, Wayne Rooney hakuwa na tatizo kubwa na hivyo yuko fiti kuelekea mchezo wa siku ya Jumatatu ambao utakuwa dhidi ya Soumpton. 

Southampton walianza ligi vizuri lakini vichapo mara mbili mfululizo kutoka kwa timu za Manchester City na Arsenal, kumeanza kutia shaka juu ya ubora wao licha ya kusalia kwenye nafasi ya tatu wakiwa na alama 26.

Wilson kuelekea mchezo huo anatajwa kuwa na nafasi kubwa ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza huku Rooney naye akirejea kikosini. 

Ni vigumu kumpeeka benchi nahodha wa timu na hivyo, Van Persie ambaye amefunga mabao manne tu msimu huu ndiye mwenye uwezekano mkubwa wa kuanzia benchi.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!