Searching...
Image and video hosting by TinyPic
2 December 2014
Tuesday, December 02, 2014

Mchezaji bora wa mwaka Tanzania kuchaguliwa.


Na Chikoti Cico.

Mtandao wa habari za michezo wa Goal.com umechagua wachezaji wa tano wanaogombania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka nchini Tanzania kwa mwaka 2014, kinyang’anyiro hicho kitaamuliwa na kura zitakazaopigwa na mashabiki mbalimbali kutoka nje na ndani ya Tanzania.

Wachezaji waliongia kwenye kinyang’anyiro hicho ni: 1. Mbwana Samata(TP- Mazembe, Taifa Stars) 2. Mrisho Ngasa(Yanga- Taifa Stars) 3. Jonas Mkude(Simba-Taifa Stars) 4. Thomas Ulimwengu(TP Mazembe- Taifa Stars) 5. Salum Abubakar(Azam - Taifa Stars)

Wachezaji hawa wa tano wamechaguliwa kutokana na kufanya vizuri kwenye ngazi ya klabu zao na timu ya taifa Taifa Stars katika michuano mbalimbali waliyocheza kwa mwaka 2014.

Kuchaguliwa kwa mchezaji bora atakayenyakuwa tuzo hiyo itakayotolewa na Goal.com utaenda sambamba na upigaji wa kura toka kwa mashabiki wa soka huku siku ya Ijumaa jioni tarehe 5 ikiwa mwisho wa upigaji kura.



0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!