Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 December 2014
Thursday, December 04, 2014

Rafinha ampatia Ballon D'or Rafiki Yake.


Na Oscar Oscar Jr

Beki wa kulia wa kimataifa wa Brazil na klabu ya Bayern Munich, Rafinha ameibuka na kutoa mtazamo wake kuhusiana na tuzo ya Ballon D'or ambayo sherehe zake zitafanyika tarehe 12 mwezi January Mwakani. 

Rafinha anadhani kuwa, Kipa wa Ujerumani na klabu ya Bayern Munich, Manuel Neuer ndiye mchezaji anayestahili tuzo hiyo mwaka huu.

Rafinha ni rafiki mkubwa sana wa Neuer hasa ikizingatiwa kuwa, wamekuwa karibu tangu wakiwa watoto wadogo. Wachezaji hao walikuwa pamoja kwenye timu ya Schalke 04 na kucheza kwa miaka mitano kabla ya kuhamia timu ya Bayern Munich ambapo wamedumu kwa miaka minne sasa.

Rafinha amesema hata kama Neuer asiposhinda tuzo hiyo, kitendo tu cha kutajwa kwenye orodha ya wachezaji watatu wa mwisho, ni heshima kubwa kwake hasa ukizingatia kuwa, ni vigumu sana kwa nafasi ya golikipa kuwemo kwenye kilinyang'anyiro hicho.

Neuer ambaye alishinda taji la Bundesliga msimu uliopita na Kombe la chama cha Soka nchini Ujerumani, alikuwa pia sehemu ya majushaa wa Ujerumani walitwaa kombe la Dunia nchini Brazil huku akionyesha kiwango cha juu.

Rafinha ni sehemu ya kikosi cha kwanza cha Bayern Munich tangu ujio wa kocha Pep Gaurdiola, amekiri pia kuwa uwepo wa mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi na mshambuliaji wa Real Madrid Christiano Ronaldo, kunapunguza uwezekano wa kipa huyo kupata Ballon D'or ingawa anadhani kuwa anastahili.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!