Searching...
Image and video hosting by TinyPic
2 February 2017
Thursday, February 02, 2017

BANCE AVUNJA REKODI MBILI KWA WAKATI MMOJA


Na FLORENCE GR

Michuano ya kombe la mataifa ya AFCON imeendelea kushika kasi nchini Gaboni ambapo usiku wa jana kulipigwa nusu fainali ya kwanza iliyowakutanisha Burkina Faso dhidi ya mafarao wa Misri katika dimba la Stade de l'amitile.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Bukina Faso Aristide Bance amekuwa mchezaji wa kwanza kufanikiwa kuifunga timu ya taifa ya misri kunako mashindano ya AFCON yanayoendelea nchini Gabon.

Mshambuliaji huyo alifanikiwa kufunga goli hilo kwa shuti kali lililompita kipa wa misri El Hadary akiwa hana cha kufanya dakika ya 72 huku likiwa ni goli la kusawazisha baada ya nyota wa As Roma Mohamed Sarah kuifungia Misri goli la kuongoza dakika ya 65.

El Hadary ambae aliingia kutokea benchi katika mchezo wa kwanza baada ya goli kipa Ahmed El Shenawy kuumia katika mchezo wa kwanza wa kundi D dhidi ya Mali alikuwa amecheza kwa dakika 409 bila kuruhusu goli huku ikiwa ni dakika 488 kwa timu ya Misri ambao walikuwa hajaruhusu goli tangu kuanza kwa mashindano hayo.

Hata hivyo katika mchezo huo Misri walifanikiwa kutinga fainali baada kushinda kwa changamoto ya mikwaju ya penati 5-3 baada ya dakika 120 kuisha kwa sare ya goli 1-1.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!