Na Chikoti Cico
Timu ya Arsenal ya Uingereza imeendelea kukumbwa na misukosuko ya majeruhi kwa wachezaji wake baada ya taarifa kutoka klabuni hapo kuthibitisha kuwa, kiungo Jack Wilshere atakaa nje kwa muda wa miezi mitatu hii ni baada ya kuumia kwenye mchezo uliopita dhidi ya Manchester United.
Taarifa kutoka timu ya Arsenal zilisema “Jack Wilshere amekuwa na mafanikio ya upasuaji kwenye kifundo cha kushoto na atakuwa nje kwa miezi mitatu inavyokadiriwa, uchunguzi wa daktari mtaalam ulithibitisha uhitaji wa operesheni na Wilshere amekuwa na upasuaji wa mafanikio kwenye kifundo chake jijini London Alhamisi mchana”
“Jack ataanza program ya kuponesha jeraha lake na timu ya wauguzi ya Arsenal, Kila mmoja klabuni anamtakiwa Jack kupona mapema na tunatarajia kumwona tena uwanjani mapema iwezekanavyo”
Kuumia kwa Wilshere kunaongeza idadi ya wachezaji ambao ni majeruhi kwa timu ya Arsenal ambao mpaka sasa beki wa kulia Mathie Debuchy, kiungo Mesuz Ozil wote wako nje huku kukiwa na taarifa ya kuumia kwa kipa Wojciech Szczesny, kiungo Mikel Arteta na mshambuliaji Danny Welbeck.
Wakati huo mshambuliaji Olivier Giroud na beki Laurent Koscielny ambao walikuwa nje kwa muda mrefu sasa wako fiti kuichezea timu hiyo ambayo mpaka sasa inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza wakiwa na alama 17.
0 comments:
Post a Comment