Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 December 2014
Monday, December 01, 2014

Yanga ilihitaji kiungo aina ya Mbrazil EMERSON DE OLIVEIRA?

 

 Na Samuel Samuel
0652464525

Kiungo mkabaji toka nchini Brazil, Emerson jana amesaini kandarasi ya mwaka mmoja kuitumikia klabu ya Yanga baada ya benchi la ufundi kuridhika na kiwango chake. 

Emerson ambaye anaimudu vyema nafasi ya kiungo wa chini kabla ya kutua nchini, alikuwa akiitumikia klabu ya Bonsucesso iliyopo ligi daraja la pili nchini Brazil katika jiji la Rio de Janeiro. 

Toka wameondoka viungo mahiri kwenye kikosi cha Jangwani , timu hiyo haijaweza kupata mrithi wa uhakika na ndio maana klabu hiyo imefikia maamuzi hayo. 

Athuman Idd na Frank Domayo waliacha pengo kubwa kwenye timu hiyo na kuifanya kupata matokeo ya kubahatisha bahatisha tu bila kuwa na soka nzuri la kuvutia. 

Mara nyingi Maximo amekuwa akikaririwa kuilalamikia nafasi hiyo. Emerson anaweza kuwa suluhisho baada ya kuonesha uwezo mkubwa kwa majaribio ya siku nne mfululizo. 

Emerson anatarajiwa kusaidiana vyema na Mnyarwanda, Haruna Niyonzima anayemiliki kiungo cha juu. Wengi walitarajia Maximo angerudi na mshambuliaji wa kati kutokana na Jaja kujitoa nafasi hiyo na kubaki nchini kwao. 

Lakini ukiangalia kiufundi, Yanga ilihitaji zaidi kiungo mkabaji kuliko mshambuliaji wa kati. Maximo katika mifumo yake anapendelea kushambulia kupitia kati sasa kama huna namba sita( kiungo mkabaji) aliyekamilika hutofanikiwa katika hilo. 

Mbuyu Twite katika mechi zake alizocheza nafasi hiyo, alionesha kupwaya katika kupandisha timu na kusaidiana na mabeki wa kati 4&5 kutengeneza ukuta imara. 

Twite ni mzuri akicheza kama beki wa kulia kuliko akipewa majukumu ya namba sita. Hivyo kuna uwezekano Yanga imetibu tatizo kwa kumpata Emerson.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!