Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 December 2014
Monday, December 01, 2014

Neymar kuwapiku Messi na Ronaldo


 Na Chikoti Cico

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil, Ronaldo de Lima amsifia nahodha wa sasa wa Brazili, Neymar huku akienda mbali zaidi na kusema anakaribia ubora wa Messi na Christiano Ronaldo.

Akiongea na gazeti la Folha de Sao Paulo la nchini Brazil, gwiji huyo wa soka alisema “ni karibu sana, ni wakati sasa kwa Neymar kuchukua nafasi yake kama aliyebora duniani, Christiano Ronaldo na Messi ni bora kwa kwasasa lakini Neymar ametokea mbali, kuja ulaya kumemsaidia”

Akiongelea kuhusu mchango wa Neymar kwa timu ya taifa ya Brazili maarufu kama Selecao de Lima alisema “Hatuna wachezaji bora wengi, tunaishi tukimtumainia Neymar ambaye ni bora sana, mzuri kwa nchi lakini nyakati nyingine tulikuwa na wachezaji wengine wengi ambao tungewategemea kuichezea timu ya Brazili”

Brazili ilimteua Dunga kuiongoza timu hiyo kwa mara ya pili baada ya kuwa na matokeo mabovu kwenye michuano ya kombe la dunia iliyofanyika nchini humo na mpaka sasa ameiongoza timu hiyo kushinda mechi sita mfululizo.

Ronaldo akiongelea uteuzi huo alisema “ngumu kusema, sipo huko na sikuulizwa kuhusu uongozi mpya, kiwewe cha 7-1 (dhidi ya Ujerumani) kinawaumiza Wabrazili, tunaona mwanzo mzuri baada ya mechi sita lakini bado tunahisi mauimivu”

“Tunataka kufuta kumbukumbu hiyo, lakini nina kumbukumbu nzuri ambayo ni ya 2012 dhidi ya Ujerumani yenyewe (kwenye fainali ya kombe la Dunia) ni bora nibaki na kumbukumbu hiyo”.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!