Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 December 2014
Thursday, December 04, 2014

Bundesliga wamekubali yaishe.




Na Oscar Oscar Jr

Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kila kitu kwa sasa kuendeshwa na Teknolojia, haiwezekani mpira ukeendelea kubaki Analojia. 

Hatimaye ligi kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga, msimu ujao itatumia Tekinolojia ya kuweza kung'amua goli kama ambavyo ligi ya Uingereza inafanya kwa sasa.

Kumekuwa na utata sana nchini Ujerumani juu na Teknolojia hiyo huku mara kadhaa klabu 36 ambazo zinaunda daraja la kwanza na la pili, zimekuwa zikivutana juu ya matumizi ya Teknolojia hiyo kwenye mchezo wa soka. 

Zoezi hilo limewahi kufeli baada ya washirika kushindwa kufikisha Theluthi tatu ya waliokubali huku nusu pekee ya wanachama ndiyo waliokuwa wakikubali matumizi ya mfumo huo mpya.

Kutokana na goli la beki wa Borussia Dortmund kukataliwa kwenye Fainali ya DFB-Pokal msimu uliopita wakati lilikuwa halali kwenye mchezo ambao Bayern Munich waliibuka washindi, kura zimerudiwa kupigwa na sasa, klabu 15 kati ya 18 zimekubali mfumo huo uanze kutumika kuanzia msimu wa 2015/2016.

Chama cha soka nchini humo tayari jana kiliweka wazi kuwa, Teknolojia ambayo kwa sasa inatumika kwenye ligi kuu nchini Uingereza itaanza kutumika kwenye Bundesliga mapema kuanzia Julai Mosi mwakani. 

Rais wa chama cha soka Ujerumani, Reinhard Rauball amekiri kuwa, Teknolojia hiyo itakuwa msaada kwa waamuzi huku moja ya viongozi wa juu akisema kuwa, itawagharimu kiasi kisichozidi Euro 8,000 kwa kila mechi ya Bundesliga.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!