Searching...
Image and video hosting by TinyPic
18 December 2014
Thursday, December 18, 2014

Hatimaye Mesut Ozil dimbani.


Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Arsenal, Mesut Ozil karibu atarejea dimbani na kuongeza nguvu kwenye kikosi cha kocha Arsene Wenger ambacho mwendo wake haueleweki. Ozil amekuwa nje tangu mwezi Octoba na sasa tayari ameanza kuonyesha dalili za kurejea dimbani.

Wakati Arsenal wakijiandaa na mechi yao dhidi ya Newcastle United wiki iliyopita, imebainika kuwa Ozil alionekana akifanya mazoezi mepesi kwenye uwanja wa mazoezi wa Gunners. 

Ozil amekuwa na mwanzo wa kusua sua tangu alipojiunga na washika Bunduki hao wa London akitokea klabu ya Real Madrid tofauti na Alexies Sanchez aliyetoka Barcelona kwani ameonekana kumudu soka la Uingereza.

Arsenal kwa sasa wanajiandaa na mchezo wao dhidi ya Liverpool siku ya Jumapili huku wakiamini kuwa kiungo Alex Oxlade-Chamberlain atakuwa fiti katika mtanange huo. 

Theo Walcott naye anaweza kusafiri kwa ajili ya mechi hiyo baada ya hali yake kuimarika huku wasiwasi pekee ukibaki kwa beki Laurent Koscielny ambaye atalazimika kusubiri ripoti ya daktari.

Kurudi kwa Ozil ni wazi kuwa kutaongezea nguvu kikosi cha Arsene Wenger ambao wamefanikiwa kutinga hatua ya 16 ya klabu bingwa Ulaya na kujikita kwenye nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi kuu. 

Tofauti yao na timu ya West Ham ambao wanakamata nafasi ya nne ni alama mbili pekee. Ozil ameendelea kusisitiza kuwa kama Arsenal wataimarika kiasi kwenye sehemu ya ulinzi, upo uwezekano wa kumaliza kwenye nafasi za juu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!