Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 December 2014
Monday, December 01, 2014

Gerrard apewa mkataba mpya na Liverpool.


Na Chikoti Cico.

Baada ya taarifa mbalimbali kuzagaa kwamba nahodha wa timu ya Liverpool Steven Gerrard anaweza kuiacha timu hiyo mwisho wa msimu huu kocha wa Liverpool athibitisha Gerrard kupewa mkataba mpya ili kuendelea kuichezea timu hiyo.

Gerrard ambaye alitimiza miaka 16 akiichezea Liverpool siku ya Jumamosi kwenye mchezo dhidi ya Stoke City ambapo aliingia kwenye dakika ya 75 akichukua nafasi ya Lucas Leiva.

Mchezo ulioisha kwa Liverpool kushinda kwa goli 1-0 na sasa, anatarajiwa kuendelea kubaki Anfield kuichezea timu hiyo baada ya kusaini mkataba huo mpya.

Akiongea na vyombo vya habari kuhusu mkataba mpya wa Gerrard kuelekea mechi dhidi ya Leicester City, kocha wa Liverpool Brendan Rodgers alisema “ amepewa mkataba hapa na ndivyo ilivyo, anastahili heshima kubwa sana na anastahili muda kuangalia hilo. Ni wakati muhimu kwenye maisha yake kuangalia atakachofanya katika hatua hii ya maisha yake”.

Gerrard kwasasa anapokea mshahara wa kiasi cha pauni 120,000 kwa wiki kutoka Liverpool jambo ambalo Brendan amesema halina maana sana kwenye uamuzi atakaouchukua kuhusu mkataba huo mpya.

Akiongelea hilo kocha huyo alisema “Kuna vitu vingi ambavyo anahitajika kuvifikiria lakini hakika haitakuwa fedha, anastahili kufikiri kuhusu alipo kwa wakati huu”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!