Searching...
Image and video hosting by TinyPic
28 January 2015
Wednesday, January 28, 2015

Mourinho apigwa faini.

Na Chikoti Cico


Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amepigwa faini ya kiasi cha pauni 25,000 na kuonywa na chama cha soka nchini Uingereza (FA) kufuatia madai ya kwamba kuna “kampeni” dhidi ya Chelsea kutoka kwa waamuzi. Mourinho alitoa madai hayo baada ya mchezo dhidi ya Southampton uliochezwa Desemba 28 ulioisha kwa sare ya goli 1-1.

Madai hayo ya Mourinho yameonekana kuwa hayakufaa na yemeleta sifa mbaya mchezoni, kamati huru iliyochunguza maneno hayo ya imegundua kwamba pia haya kumaanisha kwamba waamuzi wanazipendelea timu zingine dhidi ya Chelsea.

Taarifa ya FA kuhusiana na tukio hilo inasema “kufuatia masikilizano ya kamati huru ya urekebishaji, Jose Mourinho amepigwa faini ya pauni 25,000 baada ya kugundulika amevunja sheria ya FA kuhusiana na maoni kwa vyombo vya habari”

Mourinho mwenye umri wa miaka 52 alihudhuria masikilizano binafsi baada ya kushtakiwa kufuatia maoni hayo ambayo yalikuja baada ya Cesc Fabregas kunyimwa penati na badala yake alionyeshwa kadi ya njano kwa madai ya kujiangusha kwenye mchezo dhidi ya Southmpton.


Taarifa hiyo ya FA iliendelea kusema “Meneja wa Chelsea alikataa kwamba maoni aliyoyatoa baada ya mchezo dhidi ya Southampton Desemba 28, 2014 yalikuwa yasiyofaa na kwamba yalidai kuonyesha upendeleo kwa sehemu ya mwamuzi ama waamuzi, na kuuleta mchezo kwenye sifa mbaya”.

“Kamati huru ya marekebisho imegundua maoni yalikuwa ni uvunjaji wa sheria E3 ya FA na kwamba hayakufaa na yaliuleta mchezo kwenye sifa mbaya. Ingawa kamati haikugundua kwamba maoni yalionyesha upendeleo kwa sehemu ya mwamuzi ama waamuzi. Mr Mourinho ambayea aliomba masikilizano yasiyo binafsi pia alionywa kwa tabia za mbeleni”.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!