Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 October 2014
Monday, October 27, 2014

Uingereza yatoa makocha watatu Ballon D'or


Na Oscar Oscar Jr

Shirikisho la soka Duniani FIFA limeweka hadharani majina ya makocha bora duniani ambapo, baada ya mchujo wa mara ya kwanza yatapatikana majina matatu ambayo yatapelekwa kwa wapiga kura na mwezi January mwakani ndipo itakapobainika ni yupi aliyepigiwa kura nyingi.

Katika orodha hiyo ya awali, makocha kutoka ligi kuu ya Uingereza ni wawili tu. Kocha wa Manchester United, Loius Van Gaal, Manuel Pellegrini wa Manchester City na Jose Mourinho wa Chelsea. Orodha kamili ni kama ifuatavyo. 

Carlo Ancelotti, Antonio Conte, Pep Guardiola, Juergen Klinsmann, Joachim Loew, Jose Mourinho, Manuel Pellegrini, Alejandro Sabella, Diego Simeone, Louis van Gaal.

Mwaka huu mwezi January, dunia ilishuhudia aliyekuwa kocha wa timu ya Bayern Munich, Jupp Heynches akitunukiwa tuzo hiyo maarufu kama Ballon D'or.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!