Yanga yaendelea kuandamwa.
Na Oscar Oscar Jr
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Yanga, Said Bahanuzi ameingia tena kwenye dira za timu ya Stand United ambao walimuwania mchezaji huyo kabla ya ligi kuu Tanzania bara kuanza lakini, hawakuweza kufanikiwa kumnsa.
Bahanuzi amekosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha kocha wa Yanga, Marcio Maximo na sasa timu ya Stand United kutoka mkoa wa Shinyanga imejipanga kumpata Bahanuzi kwa mkopo endapo watafikia makubaliano na timu ya Yanga.
Stand United kwa sasa wanashika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi kuu baada kushinda michezo miwili, sare tatu na kufungwa mechi mbili katika mechi saba za awali za ligi kuu.
Mchezo wao wa nane, utakuwa ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar ambayo haijapoteza hata mchezo mmoja na wanaongoza ligi wakiwa na alama 15.
Stand United pia, wameendelea kuhusishwa na usajili wa mchezaji wa timu ya Simba, Awadhi Juma na kwa mujibu wa mkurugenzi wa benchi la ufundi wa timu hiyo, Muhibu Kanu wanaamini kuwa endapo Yanga watawaruhusu kumchukua Said Bahanuzi na Simba wakakubaliana kwenye dili la Awadhi, Stand United itaimarika na kufanya vizuri msimu huu.
Matokeo ya Stand United msimu huu.
Stand United 1-4 Ndanda Fc
Mgambo Jkt 0-1 Stand United
Simba 1-1 Stand United
Kagera Sugar 0-0 Stand United
Stand United 0-3 Yanga
Stand United 1-1 Tanzania Prisons
Stand United 1-0 Mbeya City.
0 comments:
Post a Comment