Zidane afungiwa miezi mitatu.
Na Chikoti Cico
Kiungo za zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa na Real Madrid Zinedine Zidane afungiwa na mamlaka ya soka nchini Hispania kwa kufundisha kikosi cha Real Madrid cha wachezaji wa akiba maarufu kama Castilla huku akikosa kigezo cha Leseni ya ukocha daraja la tatu kinachotakiwa kwa kazi hiyo.
Zidane ambaye alikuwa msaidizi wa kocha Carlo Ancelotti kwa kikosi cha kwanza cha Real Madrid mwaka 2013 kabla ya kuwa kocha wa Castilla B kwasasa anamiliki leseni ya UEFA daraja A ambayo ni sawasawa na ngazi ya ukocha daraja la pili hivyo anatakiwa anatakiwa kupata daraja la tatu Aprili 2015.
Zidane ambaye aliwahi kunyakua kombe la Dunia mwaka 1998 nchini Ufaransa amefungiwa pamoja na kocha mkuu Santiago Sanchez huku kosa la Sanchez likiwa ni kutumia beji yake ya ukocha kumficha Zidane kwa kukosa kigezo cha kuwa na ngazi ya ukocha daraja la tatu kigezo kichatambullika na shirikisho la soka la Hispania.
Akiongea baada ya tukio hilo Zidane alisema “ Wivu upo kila mahali hapa Hispania na ng'ambo, aliyenishitaki mimi alikuwa anataka kusikika kwenye vyombo vya habari."
Zidane aliongeza kuwa "kuna makocha wengi wenye tatizo kama la kwangu lakini, hakuna kinachotaarifiwa” Kiungo huyo wa zamani wa Juventus aliendelea kusema “Sina majuto kuandaa leseni yangu nchini Ufarasa, inafurahisha kuona bado kuna watu wachache wanaonitetea na kueleza kwamba sikuwa na nafasi maalum”
Wakati huo huo timu ya Real Madrid ina siku 10 za kuweza kukata rufaa kwa maamuzi hayo ya kumfungia Zidane kwenye kamati ya mashindano ya mahakama ya rufaa nchini Hispania.
0 comments:
Post a Comment