Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 October 2014
Monday, October 27, 2014

Wachezaji 23 wa Ballon D'or


Na Oscar Oscar Jr

Hatimaye orodha ya wachezaji wa soka ambao wanawania tuzo ya Ballon D'or, imewekwa hadharani huku Lionel Messi wa Barcelona na Christiano Ronaldo wa Real Madrid wakiwa miongoni mwa wachezaji 23 waliopendekezwa. 

Afrika bado inaendelea kuwakilishwa na kiungo wa klabu ya Manchester City, Yaya Toure, ingawa hakuna dalili kwa kiungo huyo kuibuka kidedea.

Kwa misimu mitano sasa, tuzo hiyo imekuwa ikiwashindanisha kwa karibu washambuliaji wawili wa Ligi kuu ya Hispania na wamekuwa wakipokeza lakini msimu huu, wanaonekena kukabiliana na changamoto kutoka kwa baadhi ya wachezaji wa Ujerumani ambao walifanya vizuri kwenye Bundesliga na kombe la Dunia huku, Arjen Robben naye wa Uholanzi akipigiwa chepuo.

Tuzo hiyo iko mikononi mwa Christiano Ronaldo na baada ya kupitia majina hayo, FIFA itabakiza majina matatu ambayo yatapigiwa kura kwa nchi wanachama wa FIFA na mwezi January mwakani, atatangazwa mchezaji ambaye atakuwa ameshinda tuzo hiyo kubwa Duniani.

Orodha kamili ya wachezaji 23 waliopendekezwa.

Gareth Bale (Wales), Karim Benzema (France), Diego Costa (Spain), Thibaut Courtois (Belgium), Cristiano Ronaldo (Portugal), Angel Di Maria (Argentina), Mario Goetze (Germany), Eden Hazard (Belgium), Zlatan Ibrahimovic (Sweden), Andres Iniesta (Spain), Toni Kroos (Germany), Philipp Lahm (Germany), Javier Mascherano (Argentina), Lionel Messi (Argentina).

Wengine ni Thomas Mueller (Germany), Manuel Neuer (Germany), Neymar (Brazil), Paul Pogba (France), Sergio Ramos (Spain), Arjen Robben (Netherlands), James Rodriguez (Colombia), Bastian Schweinsteiger (Germany), Yaya Toure (Côte d’Ivoire).

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!