Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 March 2014
Thursday, March 27, 2014

MAN CITY KUIZIKA ARSENAL KESHO.


Manchester City wamejiandaa kuuwa ndege wawili kwa jiwe moja mwishoni mwa juma hili pale watakapo ongeza presha kwa vinara wa ligi hiyo klabu ya Chelsea na kufuta kabisa ndoto za klabu ya Arsenal kuweza kutwaa taji hilo. 

Ushindi wa bao 3-0 walioupata siku ya jumanne katika jiji la Manchester dhidi ya mahasimu wao,timu ya Man United,uliwafanya waikaribie Chelsea kwa tofauti ya alama 3 huku wakiwa na michezo miwili mkononi.Man City ndiyo timu inayopewa nafasi kubwa ya kumaliza mbio hizo za ligi kuu kama vinara.

Arsenal wako nyuma ya watoto hao wa Kocha Pellegrin kwa alama 3 huku wakiwa wamecheza michezo miwili zaidi na hawatotaka kabisa kupoteza mchezo wao pale timu hizo zitakapo kutana katika Uwanja wa Emirates jumamosi hii.


Baada ya kudharirishwa na Chelsea kwa kupigwa bao 6-0 wiki iliyopita,Arsenal walijikuta wakijifunga goli dakika za majeruhi na kufanya mchezo kumalizika kwa sare ya kufungana bao 2-2 na timu ya Swansea City siku ya jumanne,na endapo watafungwa na Man City,matumaini ya kutwaa taji hilo,yatakuwa yamepotea rasmi.




Arsenal imekuwa timu ambayo inafungwa magoli mengi sana dakika za awali za mchezo ukirejerea mchezo wake na Chelsea na ule wa mwezi uliopita dhidi ya Liverpool walipolala bao 5-1,na pia waliweza kufungwa bao 6-3 na Man city pale walipotembelea dimba la Etihad.Kiungo wa Gunnners Methew Flamini amesema hawatoweza kukubali kuanza vibaya tena kuelekea mchezo huo.

"Tunatakiwa kuwa waangalifu sana kwenye safu yetu ya ulinzi,kwa sababu,unapocheza na timu kubwa hasa ambayo iko vizuri katika ushambuliaji,hilo ndiyo huwa jambo la msingi" Alisema Mfaransa huyo ambaye goli lake la kujifunga lilisababisha sare dhidi ya Swansea katikatika ya wiki. aliiambia tovuti ya klabu hiyo.



RATIBA
 
JUMAMOSI
Arsenal v Manchester City
Crystal Palace v Chelsea
Manchester United v Aston Villa
Southampton v Newcastle United
Stoke City v Hull City
Swansea City v Norwich City
West Bromwich Albion v Cardiff City

 
JUMAPILI
Fulham v Everton
Liverpool v Tottenham Hotspur

 
JUMATATU
Sunderland v West Ham United

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!