Arsenal kupata nguvu nyingine dhidi ya QPR
Na Florence George
Kiungo wa kimataifa wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Wales Aaron Ramsey anatarajiwa kurejea uwanjani siku ya jumatano pale timu yake itakapokuwa ikimenyana na timu ya QPR katika mechi ya ligi kuu nchini Ungereza.
Mchezaji huyo alikosekana katika michezo minne iliyopita ambayo Arsenal ilicheza ambapo alikuwa akisumbuliwa na majeruhi ambayo yamekuwa yakimsumbua mara kwa mara msimu huu hadi kudaiwa kushuka kiwango.
Hayo yamethibitishwa na kocha wa Arsenal Arsene Wenger pale alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuelekea mchezo wao dhidi ya QPR,ambapo alisema kuwa "Ramsey amerudi na atakuwepo kwenye timu itayoenda kupambana na QPR".
Akizungumzia kama kuna uwezekano wa Francis Coquelin kucheza mchezo huo,Wenger alisema kuwa "Coquelin atafanya mazoezi leo na sioni sababu ya kutocheza mchezo huo.Atatakiwa kuvaa kifaa maalumu(mask) kama akicheza".
Arsenal ambayo jumapili iliibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Everton,mpaka sasa inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 51 katika michezo 27 iliyocheza mpaka sasa pointi moja mbele ya Manchester United iliyonafasi ya nne huku ikizidiwa pointi 9 dhidi ya vinara wa ligi hiyo timu ya Chelsea yenye pointi 60 katika michezo 26 iliyocheza hadi sasa.
0 comments:
Post a Comment