Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 October 2014
Monday, October 27, 2014

Rooney aumia tena na kuikosa Manchester City




Na Oscar Oscar Jr

Kuna habari ambazo sio nzuri hasa kwa mashabiki wa timu ya Manchester United kufuatia kuumia kwa Nahodha wa timu hiyo Wayne Rooney huku timu hiyo ikiwa inajiandaa na mchezo wa Manchester Derby utakaopigwa weekend hii dhidi ya Manchester City kwenye dimba la machinjio, Etihad.

Rooney alikaa nje kwa mechi tatu kufuatia kupewa kadi nyekundu na kukosa moja ya mchezo mgumu na muhimu kwao wa juma lililopita dhidi ya Chelsea ambapo goli la dakika za lala salama kutoka kwa Robin Van Persie, liliokoa jahazi na kupata sare ya kufungana 1-1.

Taarifa zilizotoka ni kuwa, Mshambuliaji huyo ameumia na huenda akaukosa mchezo dhidi ya Manchester City. Kabla ya kuwavaa Chelsea, Kocha Loius Van Gaal alimkosa mshambuliaji Radamel Falcao kutokana na kuumia mazoezini dakika za mwisho lakini, kuna habari njema kuwa star huyo wa Colombia atakuwa fiti dhidi ya Manchester City.

Manchester United wako kwenye nafasi ya nane wakiwa na pointi 13, huku wakionekana kutopoteza mchezo wowote tangu walipomkosa nahodha wao Rooney. Watapambana na Manchester City ambao wako kwenye nafasi ya tatu wakiwa na pointi 17.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!