Searching...
Image and video hosting by TinyPic
28 October 2014
Tuesday, October 28, 2014

Pellegini kumpeleka Semi Khedira Etihad


Na Rossa Kabwine

Timu ya Manchester city wameingia katika mbio za kumuwania kiungo wa Ujerumani na Real Madrid, Sami Khedira. Mchezaji huyo ni moja kati ya wachezaji wanao takiwa sana katika dirisha la usajili la Januari na timu za Arsenal, Chelsea, Liverpool na Manchester united.

Timu hizo zote zimeonesha nia ya kuhitaji huduma ya kiungo huyo ambaye alishinda kombe la klabu bingwa Ulaya msimu uliopita akiwa na Real Madrid na kombe la Dunia, akiwa timu ya taifa ya Ujerumani.

Kuna taafifa kuwa klabu ya Real Madrid na Khedira wameshindwa kukubaliana masharti katika mkataba mpya na klabu hiyo, inafikiria kumuuza mchezaji huyo dirisha la usajiri litakapofunguliwa.

Ripoti zinasema mabingwa wa uingereza, Manchester city wana mtaka khedira na wanataka kumsajili majira ya baridi. Wiki iliyopita iliripotiwa kuwa khedira mwenye umri wa miaka 27 kuwa anajitayarisha kupunguza mshahara wake ili aweze kuondoka Real madrid.

Meneja wa Madrid, Carlo Ancelotti siku za karibuni alisema, ana matumaini ya kumbakiza khedira na alijaribu kuondoa uvumi wa kiungo huyo kuondoka januari akisema “ tuna muda hadi juni wa kufikia makubaliano naye" 

Kocha huyo aliongeza  kuwa “ kama anataka kuongeza mkataba, klabu itamuongezea. kama sio, ataondoka mwisho wa msimu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!