Searching...
Image and video hosting by TinyPic
28 October 2014
Tuesday, October 28, 2014

Pep Gaurdiola amshika mwamuzi mwanamke.



Na Oscar Oscar Jr 


Kocha wa timu ya Bayern Munich, Pep Gaurdiola anaweza kujikuta akifungiwa mechi kadhaa kutokana na kosa la kuvuka eneo ambalo makocha wanaruhusiwa kutawala wakati wa mchezo. 

Tukio hilo limetokea kwenye mchezo wa Bundesliga ambapo Bayern Munich walitoka sare tasa na Borussia Monchengladbach.

Kocha huyo alijikuta akimvamia mwamuzi msaidizi wa kike katika eneo lake na kuomba dakika za nyongeza na kumgusa mwamuzi huyo wa nne wa mchezo huo jambo ambalo, ni kinyume na kanuni za ligi kuu nchini Ujerumani. 

Mwanamama huyo anayeitwa  Bibiana Steinhaus , alishituka baada ya kuona Pep akimuwekea mkono shingoni.

Bayern Munich wanaongoza ligi ya Bundesliga wakiwa na alama 21 baada ya kushuka dimbani mara tisa. Mshambuliaji Mario Gotze wa Bayern anaongoza kwa kufunga magoli sita huku timu hiyo ikiwa imeruhusu nyavu zake kutikiswa kwa mabao mawili pekee.

Kocha huyo raia wa Hispania ambaye alishinda mataji mengi akiwa na Barcelona, atalazimika kusubiri uamuzi wa DFB chama cha soka nchini Ujerumani ili kujua hatima yake kwani kanuni za ligi hiyo haziruhusu kocha kugusana na mwamuzi.





0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!