Mourinho amlaumu kocha wa Hispania kuhusu Diego Costa.
Na Oscar Oscar Jr
Kocha wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho ameibuka na kumlaumu kocha wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque kwa tatizo la mshambuliaji Diego Costa.
Mshambuliaji huyo alianza na kasi ya hatari katika kupachika mabao na kwenye mechi saba za awali, tayari alikuwa amefunga magoli tisa.
Mourinho ameibuka na kudai kuwa, kitendo cha Vicente del Bosque kumuanzisha mshambuliaji huyo mfululizo kwenye mechi za Slovakia na Luxembourg mwanzoni mwa mwezi wa kumi, ndiyo chanzo cha mshambuliaji huyo kutokuwa fiti.
Costa alikuwa aanze kwenye kikosi cha Chelsea kilichotoka sare ya kufungana bao 1-1 na Manchester United lakini baada ya kuanza kupasha misuli, Mshambuliaji huyo aliyewagharimu Pauni 30M alishindwa kuwa sawa na nafasi yake kuchukuliwa na Didier Drogba.
Mourinho amethibitisha kuwa Costa hawezi kusafiri kuelekea mechi yao na timu ya Shrewsburykwenye Capital One Cup lakini, atakuwa fiti kuwakabili timu ya QPR mwishoni mwa juma hili kwenye muendelezo wa mechi za Ligi kuu Uingereza ambapo Chelsea anaongoza akiwa na pointi 23.
0 comments:
Post a Comment