Searching...
Image and video hosting by TinyPic
30 October 2014
Thursday, October 30, 2014

Marco Reus kutua Anfield.




Na Oscar Oscar Jr

Kiungo wa kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Borussia Dortimund, Marco Reus ameripotiwa kutaka  kujiunga na timu ya Liverpool kufuatia majadiliano ya kuongeza mkataba mpya na timu yake kutofikia muafaka.

Borussia Dortimund kwa sasa hawafanyi vizuri kwenye ligi ya Bundesliga na  wanashika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi hiyo wakiwa na alama saba pekee baada ya michezo tisa ya awali. Liverpool wanadaiwa kuandaa kitita cha Pauni 32M huku mshahara wa Pauni 180,000 ukitajwa kumleta Star huyo Anfield.

Liverpool ambao wako kwenye nafasi ya saba kwenye ligi kuu Uingereza, wanataka kuongeza nguvu kwenye safu yao ya ushambuliaji ambayo inaonekana kusua sua mara baada ya Luiz Suarez kutimkia zake Barcelona. 

Reus pia anahusishwa na klabu ya Bayern Munich ambao kwa kipindi cha hivi karibuni, wamekuwa na tabia ya kuibomoa Dortimund kwa kuchukuwa wachezaji wake muhimu. 

Kiungo Mshambuliaji, Mario Gotze na mshambuliaji Robert Lewandowski ni miongoni mwa wachezaji walioikacha Dortimund na kutua kwa The Bavarians.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!