Bayern na Chelsea ndiyo kikwazo kwa Real Madrid.
Na Abuu Hussein
Msimu wa 2014 - 2015 wa Mashindano ya Klabu bigwa barani ulaya, umeendelea juzi na jana usiku kwa michezo mbalimbali kuchezo huku timu na wachezaji mbalimbali wakiweka rekodi Ama kuzifikia.
Moja ya rekodi hizo ni ile ileyokuwa ikiwaniwa na wachezaji nguli wawili duniani Leonel Messi na Cristiano Ronaldo, kufikisha goli 71 sawa na Raul Gonzalez mchezaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid.
Tayari Messi amembwaga mpinzani wake, Christiano Ronaldo kwa kuwa wa kwanza kuifikia rekodi hiyo ya magoli 71 na kumwacha Ronaldo akibakiwa na magoli 70.
Kwa upande wa vilabu kuna rekodi mmoja kubwa ambayo tokea mashindano hayo yalipobadilishwa jina na kuitwa klabu bingwa barani ulaya, hakuna timu iliyowahi kulitwaa taji hilo mara mbili mfululizo.
Msimu huu mambo yanaweza kuwa tofauti na kupelekea rekodi hiyo kuvunjwa na mabingwa watetezi Real Madrid hasa kuzingatia mambo yafuatayo.
Kiwango bora kiuchezaji kinachoonesha na timu hiyo baada ya kuanza vibaya kwenye la liga kwa kufungwa michezo miwili na kujirekebisha hadi kwa kushinda michezo yao yote iliyofuata ya la liga pamoja na klabu bingwa ulaya na kuwashusha wapinzani wao Barcelona kutoka kileleni mwa msimamo wa ligi hadi nafasi ya nne.
Pia, kucheza kwa kujiamini kumesaidia kupunguza pressure ya kupoteza mchezo hasa kwa kuzingatia kuwa Ronaldo, amekuwa ndo muhumili wa ushindi kwa timu ikiwa ni pamoja na kufanga magoli mengi na kutengeneza magoli ambapo mpaka sasa anaongoza kwa magoli La Liga akiwa ameshafunga mabao 17.
Bado Ronaldo anatamaa ya kuvunja na kuweka rekodi mbalimbali kitu ambacho kwa timu ni faida kubwa, mfano jana alipokuwa akikabiziwa tuzo ya mfungaji bora wa ulaya aliyotwaa pamoja na Luis Suarez alinukuliwa akisema:
" Natamani kuwa mchezaji bora zaidi duniani pamoja na kuisaidia timu yangu kuchukua mataji mengi zaidi kadri iwezekanavyo'.
Bayern Munich na Chelsea ndiyo timu pekee zenye uwezo wa kuizuia madrid isitetee taji lake la klabu bingwa barani ulaya kutokana na ubora wa makocha walionao na ubora timu walizonazo.
Bayern Munchen chini ya Pep Guardiola ndio timu yenye nafasi kubwa zaidi kuwatibulia Real Madrid kutokana na ubora wa kikosi chao bila kusahau,uwezo mkubwa wa mwalimu wao Gardiola katika mbinu za kufundisha timu na kuwasoma wapinzani.
Pep ni kocha anayetaka pia kuongeza rekodi yake kwa kuipa Bayern Munich taji la klabu bingwa ulaya baada ya kuipa Barcelona taji hilo mara mbili.
Chelsea ni timu nyingine yenye uwezo wa kuwatibulia Real Madrid kujiandikia rekodi ya kuchukua ubingwa wa ulaya mara mbili mfululizo hasa kwa ubora mbinu alizonazo kocha wake Jose Morinho pamoja na kuifahamu vizuri real madrid kuna weza kuchangia kuisimamisha madrid.
Chelsea ndiyo timu yenye mbinu nzuri zaidi ya kucheza na timu zenye uwezo wa mkubwa wa kumiliki mipira na kupigaa pasi nyingi. Kumbukumbu zinaonyesha kuwa, chelsea imeshazibwaga Bayern Munich na Barcelona kisha ikalitwaa taji hilo bila kujali uwezo wa timu hizo katika kumiliki mpira.
Jambo la mwisho kwa chelsea, ni uwepo wa Mourinho ambaye ndiye kocha mwasisi wa mbinu ya kupaki basi. Tusubiri tuone kama madrid atafanikiwa kuliteta taji lake la klabu bingwa ulaya na kujiwekea rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuimarika kwa mbinu pamoja na kuongezeka viwango vya kiuchezaji kwa timu pamoja na mchezaji mmoja mmoja.
0 comments:
Post a Comment