Searching...
Image and video hosting by TinyPic
28 December 2014
Sunday, December 28, 2014

Ancelotti awania tuzo ya dunia.


Na Chikoti Cico

Kocha wa timu ya Real Madrid, Mwitaliano Carlo Ancelotti anawania tuzo ya kocha bora kwa mwaka 2014 inayotolewa na Globe Soccer baada ya kuiongoza timu hiyo inayoshiriki ligi ya Hispania maarufu kama la liga kunyakua kombe la klabu bingwa barani Ulaya likiwa ni kombe la kumi (la decima) kwa timu hiyo.

Ancelotti aliyechukua nafasi ya Jose Mourinho kuifundisha timu ya Real Madrid pia aliziongoza timu kama AC Milan, Chelsea na PSG kwa mafanikio makubwa huku akifanikiwa kuchukua makombe mbalimbali wakati akizifundisha timu hizo.

Kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo hiyo Ancelotti anashindana na kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Low aliyeiongoza timu hiyo kunyakua kombe la dunia, pia yupo kocha wa Bayern Munich Pep Guadiola aliyeongoza timu hiyo kunyakua makombe mawili kwenye msimu wake wa kwanza.

Huku pia Kocha wa zamani wa Juventus Antonio Conte akiwania tuzo hiyo baada ya kuiongoza Juventus kunyakua kombe la ligi ya Seria A mara tatu mfululizo kabla ya kuachia ngazi na kwenda kuifundisha timu ya taifa ya Italia.

Ancelloti ambaye mpaka sasa ameiongoza timu ya Madrid kushinda michezo 23 mfululizo kwenye mashindano mbalimbali anatarajia kuhudhuria hafla ya ugawaji wa tuzo itakayofanyika kwenye hoteli ya Palm jijini Dubai hapo Desemba 29.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!