Na Chikoti Cico
Baada ya michezo ya Capital One Cup kuchezwa katikati ya wiki hii huku timu mbalimbali zikicheza hatimaye ligi kuu ya Uingereza imerejea tena huku moja ya mechi zitakazochezwa Jumamosi ni kati ya Chelsea dhidi ya QPR mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Stamford Brdge jijini London.
Chelsea waliotoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Manchester United katika mchezo uliopita wataingia kwenye mchezo huo kutaka kuendeleza rekodi ya kutofungwa mpaka sasa kwenye ligi kuu ya Uingereza huku wakiwa wamecheza michezo tisa na kushinda michezo saba huku wakitoka sare michezo miwili.
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho ataendela kuwakosa mshambuliaji Loic Remy aliyeko majeruhi na beki Cesar Azpilicueta ambaye anatumikia adhabu ya kukosa michezo mitatu baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Crystal Palace na huu utakuwa mchezo wake wa mwisho kuukosa kwa beki huyo.
Wakati huo huo, habari njema kwa mashabiki wa Chelsea ni kurejea kwa mshambuliaji Diego Costa na kiungo Ramirez waliokuwa majeruhi.
Takwimu zinaonyesha mpaka sasa Chelsea imecheza michezo minne nyumbani na kushinda yote huku ikifunga magoli 11 na kufungwa magoli mawili pekee.
kikosi cha Chelsea kinaweza kuwa hivi: Courtois; Ivanovic, Terry, Cahill, Luis; Matic, Fabregas; Hazard, Oscar, Willian; Costa
Kwa upande wa QPR Kocha Harry Rednapp anatarajiwa kuingia kwenye mechi hii kutafuta ushindi wa kwanza ugenini kwani mpaka sasa katika mechi nne QPR walizocheza ugenini, zote wamepoteza.
Kocha Rednapp atawakosa Alejandro Faurlin, Joey Barton na Jordan Mutch ambao ni majeruhi pia watamkosa beki Rio Ferdinand aliiyefungiwa na chama cha soka cha Uingereza FA kwa matumizi mbaya ya lugha kwenye mtandano wa tweeter.
QPR ambao wanashika nafasi ya 19 wakiwa na alama saba kati ya michezo tisa waliocheza bado wanajikongoja kutoka mkiani kwenye msimamo wa ligi huku wakiwa wameshinda michezo tisa na kutoka sare mchezo mmoja huku wakiwa wamepoteza michezo sita na takwimu zinaonyesha mpaka sasa, wamefunga magoli nane na kufungwa magoli 18.
Kikosi cha QPR kinaweza kuwa hivi: Green; Isla, Dunne, Caulker, Yun; Fer, Sandro, Henry; Vargas, Hoilett, Austin
0 comments:
Post a Comment