Searching...
Image and video hosting by TinyPic
11 January 2015
Sunday, January 11, 2015

Uchambuzi: Mgambo JKT VS RUVU SHOOTING.


Na Oscar Oscar Jr

Mgambo JKT kutoka Tanga leo hii itawaalika Ruvu Shooting kutoka mkoa wa Pwani kwenye mchezo wa mzunguko wa 10 wa ligi kuu Tanzania bara kwenye dimba la Mkwakwani majira ya saa 10:30 Jioni.

Kuelekea mchezo huo, Mgambo wana pointi tisa huku wakiwa na ushindi mara tatu na tayari wamepoteza mechi tano na bado wanamchezo mmoja mkononi ambao wataucheza dhidi ya timu ya Simba inayoshiriki Mapinduzi Cup huko Zanzibar.

Kwa upande wa Ruvu Shooting ambao wameshashuka dimbani mara tisa, wamejikusanyia alama 11 huku wakishinda mechi tatu, sare mechi mbili na kupoteza mechi nne na kushika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi kuu.

Endapo Ruvu Shooting wataibuka na ushindi kwenye mchezo huo, watafikisha alama 14 ambazo zimefikiwa na timu za Kagera Sugar, Azam Fc, na Yanga. 

Kwa upande wa Mgambo wao ushindi kwenye mchezo huu utawafanya watimize alama 12 na hivyo kujiondoa kwenye timu tatu za chini kwenye msimamo wa ligi hiyo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!