Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 December 2014
Saturday, December 27, 2014

Ronaldo haendi kokote.


Na Chikoti Cico
 
Mchezaji bora wa dunia mara mbili, Christiano Ronaldo anayeichezea timu ya Real Madrid haendi kokote na atastaafu soka akiwa anaichezea timu hiyo kutoka jiji la Madrid ndivyo ambavyo wakala wake alivyosema hasa baada ya Ronaldo kuhuishwa kurejea timu yake ya zamani ya Manchester United mara kwa mara.

Wakala wa mchezaji huyo kutoka Ureno, Jorge Mendes amesema Ronaldo ataendelea kuichezea Real Madrid mpaka siku atakayoamua kuachana kabisa na mchezo wa soka, Ronaldo ana mkataba na Madrid mpaka Juni 2018 ambapo wakati huo atakuwa na miaka 33.

Akiongea na Globo Esporte Mendes alisema “ nilipata kumjua akiwa na miaka 15, kutokea hapo mpaka sasa tumekuwa tukizungumza mara nyingi, nikiwa Madrid huwa tunakutana, uhusiano wetu zaidi ni kama urafiki.

Ninaamini kwamba Christiano atamalizia soka lake Real Madrid, anafuraha klabuni hapo na bado ana hamu ya kufanikiwa zaidi hapo Madrid”.

Aliendelea kumsifia mcheziji huyo akisema “klabu itaweza kustaafisha jezi yake atakapomalizia soka lake Madrid. Kwa kila heshima kwa Raul na Di Stefano hakuna mchezaji wa kumfananisha na Christiano Ronaldo.

Ni mchezaji bora kwenye historian a niseme mwanamichezo bora bora wa muda wote, hatutamwona mwingine kama Christiano tena itakuwa ni vigumu kabisa”.

Alipoulizwa kama Ronaldo ataweza kushinda tuzo ya Ballon dOr mara nne zaidi ya Messi Mendes alijibu “kama ataendelea kuwa fiti, nina hakika atabaki kubwa bora kwa muda”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!