Na Oscar Oscar Jr
Beki wa kati wa kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Borussia Dortmund, Mats Hummels ameonekana kuikataa klabu ya Manchester United na kutaka kujiunga na timu ya Arsenal.
Muendelezo wa wachezaji mastaa wa Borussia Dortmund kuikacha klabu hiyo, umeendelea kupamba moto. Kiungo wa timu hiyo Marco Reus naye anahusishwa kuhamia klabu za Liverpool na Bayern Munich. Taarifa hii ni kwa mujibu wa Gazeti la Sunday Mirror
Klabu za Manchester United, Tottenham na Arsenal zimeendelea kutajwa kuwania saini ya beki wa kulia wa kimataifa wa Brazil na klabu ya Barcelona, Dani Alves.
Beki huyo anaonekana kutokuwa kwenye mipango ya kocha mpya wa Barcelona, Luiz Enrique na hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kuweza kuuzwa mwezi January. Taarifa hii ni kwa mujibu wa Gazeti la Sunday Times.
Klabu ya Real Madrid imejipanga kumuuza winga wa kimataifa wa Wales, Gareth Bale January kwenda klabu ya Manchester United huku taarifa zikieleza kuwa, Mabingwa hao wa Ulaya wanataka kumsajili kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ugelgiji, Eden Hazard kutoka klabu ya Chelsea. Habari hii ni kwa mujibu wa Gazeti la Metro.
Klabu ya Liverpool, inajiandaa kumchukuwa Golikipa wa timu ya Stoke City, Asmir Begovic ili aweze kumletea changamoto golikipa wa sasa wa timu hiyo, Simon Mignolet ambaye anaonekana kusua sua huku akifungwa magoli mepesi kabisa. Taarifa hii ni kwa mujibu wa Gazeti la Sunday Mirror
0 comments:
Post a Comment