huu ni ushindi ambao sio ushindi.
mwaka 2012 bingwa wa EPL alipatikana mechi ya mwisho.united alikuwa anamaliza na sunderland pale Stadium of Light na akashinda 1-0,Fergie na wanae waliendelea kubaki uwanjani huku wakisubiri matokeo ya Etihad.Sekunde ya za mwisho Kun Aguero akawapa city goli la ubingwa.pamoja na kuwa Fergie na wanae walishinda lakini hawakuwa na furaha na ushindi wao,taratibu wakapotea uwanjani.
Barcelona vs Inter millan
mwaka 2010 Mourinho kwenye mechi ya kwanza aliwasambaratisha Barca 3-1 pale GEUSEPE MEAZZA,baada ya wiki moja walirudiana pale Camp Nou na Barca akashinda 1-0.pamoja na kuwa barca walishinda,baada ya mechi Mourinho alikuwa akishangilia na wao wanalia.
Arsenal vs Ac Millan
mwaka 2012 arsenal alifanyiwa kitu mbaya pale San Siro baada ya kupigwa 4-0 na ac millan.mechi ya marudiano pale Emirates kipindi cha kwanza tu,arsenal alikuwa anaongoza 3-0.mwisho wa mchezo,pamoja na ushindi wa arsenal wao ndo walibaki wameinama,millani wanatabasamu.
Real madrid vs Dortmund
mourinho hatomsahau Lewandowski baada ya kumfunga 4-1 pale Signal Iduna Park ujerumani baada ya wiki moja walirudiana pale Bernabeu na madrid akashinda 2-0.mwisho wa mechi,Madrid wanalia, watoto wa "black and yellow" wanashangilia
huu ni ushindi ambao sio ushindi.
0 comments:
Post a Comment