Oliver Giroud nje mechi ya Besiktas
Na Chicoti (Cico cicod)
0755 700 076
Kocha Arsene Wenger anaweza kumkosa mshambuliaji wake Oliver Giroud baada ya kuvunjika mguu kwenye mechi dhidi ya Everton iliyoisha kwa sare ya magoli 2-2 huku Giroud akiisawazishia timu ya Arsenal dakika ya 90.
Taarifa za awali zinasema Giroud anaweza kuwa nje kwa miezi mitatu. Kuumia kwa Giroud kunaweza kumlazimisha kocha Arsene Wenger kusitisha dili la kumuuza Lucas Podolski ambaye anatakiwa na timu kama Wolfsburg na Galatasary ama itamlazimu Wenger kuingia sokoni na kufanya usajili wa mshambuliaji mwingine kabla ya kipindi cha usajili kumalizika.
kuumia kwa Giroud kutasababisha akae nje ya uwanja kwa muda mrefu. Wenger anaweza kurejea kumsajili mshambuliaji Loic Remy kutoka QPR, usajili ambao ulikaribia kukamilika mapema wakati dirisha la usajili lilipofunguliwa.
Moja ya sababu za Arsenal kushindwa kumsajili mfaransa huyo ni madai yake ya mshahara wa pauni 90,000 kwa wiki. Giroud alitarajiwa angekuwa fiti kwa mechi ya marejeano ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Besiktas ya Uturuki ila taarifa zinasema anaweza kukosa mechi hiyo ya mtoano itakayopigwa kwenye uwanja wa Emirates.
Taarifa kamili juu ya kuumia kwa Giroud na ni kwa muda gani atakaa nje zinatarajiwa kutolewa leo (Jumanne) wakati kocha Wenger atakapoongea na waandishi kuelekea mechi ya Jumatano dhidi ya Besiktas.
0 comments:
Post a Comment