Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 October 2014
Monday, October 27, 2014

Big up Mtibwa Sugar


Na Oscar Oscar Jr

Vijana kutoka mkoani Morogoro, timu ya Mtibwa Sugar imeendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kujipatia ushindi kwenye mchezo wao dhidi ya Mbeya City uliopigwa kwenye dimba la Sokoine jijini Mbeya kwa mabao 2-0.

Mabingwa hao wa ligi kuu bara mwaka 1999 na 2000, walianza vema kampeni yao ya ligi kuu kwa kupata ushindi mbele ya timu ya Yanga kwenye mchezo wao wa kwanza na baadaye, walifanikiwa kuwafunga Ndanda fc na Mgambo Jkt.

Ushindi huo wa jana, umewafanya watimize alama 13 na kuwaacha Azam na Yanga wakiwa na alama 10 kila mmoja. Mwanzo mzuri wa timu hiyo ya kocha mzawa Mecky Mexime, umechangiwa na team work ya  kila mtu anayehusika na ubora wa washambuliaji wake Ame Ally na Ally Shomary ambao kila mmoja amefunga magoli matatu.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!