Searching...
Image and video hosting by TinyPic
10 January 2015
Saturday, January 10, 2015

Ruvu JKT wafungana pointi kileleni na Mtibwa Sugar


Na Oscar Oscar Jr

Stand United imepoteza mchezo wake wa tatu msimu huu na wakwanza ugenini mbele ya Ruvu Jkt mchezo uliopigwa Jioni hii kwenye dimba la Azam Complex Jijini Dar es Salaam. 

Stand United ambao walikuwa nafasi ya tisa kabla ya mchezo huo, wamelala kwa bao 2-1 mbe ya vijana wa kocha Felix Minziro.

Jkt Ruvu wanaonekana kuwa tishio kwa sasa kufuatia kupata ushindi mfululizo baada ya wiki iliyopita kuwalaza bao 1-0 Coastal Union Jijini Tanga.

Kwa ushindi wao wa leo Ruvu wamekufungana pointi (16) na vinara wa ligi hiyo timu ya Mtibwa Sugar ambayo inashiriki michuano ya Mapinduzi Cup kule visiwani Zanzibar licha ya kuwa Ruvu wamecheza mechi nyingi za ligi kuu kuliko Mtibwa Sugar.

Stand United wanajiandaa kuanza safari ya kurejea mkoani Shinyanga siku ya kesho baada ya kucheza mechi tatu mfululizo ugenini huku wakitoka sare dhidi ya Mtibwa Sugar, Polis Moro kabla ya kupoteza mchezo wao wa leo dhdi ya JKT Ruvu.

Wakiwa katika dimba la Kambarage Shinyanga, Stand United wiki ijayo watakuwa na kibarua cha kuvaana na mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara, timu ya Azam ambayo imetoka kufungasha virago kwenye hatua ya robo fainali ya Mapinduzi Cup inayoendelea visiwani Zanzibar.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!