wakati mwingine huenda mtu asione umuhimu wa kadi nyekundu lakini hapa unaweza kuona madhara yake na namna inavyoweza kuiathili timu inapotaka ushindi.
msimu huu unaomalizika pale EPL,spurs walikutana na Arsenal Emirates na wakawa wametawala mchezo na Adebayor kawa kawa akaendeleza rekodi yake ya kuifunga timu yake hiyo ya zamani.baadae alipewa kadi nyekundu.baada ya kadi hiyo,timu yote ilipoteza mwelekeo na mwisho wa dakika 90 wakawa wamechezea kichapo cha 5-2.
mwaka 2009 united walikutana na BAVARIANS kule ARIANZE ARENA kwenye UCL na wakafungwa 2-1 na mechi ya marudiano united wakikuwa moto wa hatari pale OT ila baada ya RAFAEL kupewa kadi nyekundu iliwafanya BAYERN wapate goli na kufanya mechi kumalizika kwa united kushinda 3-2 na wakaondolewa.
msimu huu tumeshuhudia nguvu ya kadi nyekundu pale Man u walipowakaribisha Madrid katika uwanja wa OT.united walitawala kila kitu na kwa goli la kujifunga kwa madrid liliipa faida kubwa manchester lakini,baada ya kadi nyekundu ya NANI unaweza kuona namna mambo yalivyobadilika na kufanya united kuondolewa mashindanoni.
hivi ndivyo kadi nyekundu inavyoweza kuitoa timu mashindanoni.
18 May 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment