Searching...
Image and video hosting by TinyPic
24 May 2013
Friday, May 24, 2013

NIONAVYO MIMI WEMBLEY SPECIAL

                                               

Bavarians mara ya mwisho walipata ubingwa mwaka 2001 na kwa hivi karibuni wameweza kufika fainal mara 3 ndani ya misimu 4 na kupoteza 2 na leo kama watapoteza,itakuwa ya 3 .wanapata sana magoli kutokea pembeni kwa ama ARJEN ROBEN au FRANK RIBERY.hawa jamaa wanasumbua sana pembeni mwa uwanja na kuna uwezekano LUKAS PISZECZECK ambaye atakuwa upande wa RIBERY atapata tabu sana huku schemezer akikumbanA na ROBEN.

BAVARIANS wamekuwa na msimu mzuri sana huku JAVI MARTINEZ NA SCHWEINSTIGER waking'arisha sana kwenye kiungo.wanakikosi kikubwa ndomaana leo hii huwezi hata kustuka kwamba TONI KROOS NA BADSTUBER hawamo kikosini.
                                                

DORTIMUND wamejipanga na wanataka kufuta machungu ya kupoteza ubingwa wa BUNDASLIGA kwa mahasimu wao BAVARIANS.HUMMELS anaonekana anawezacheza ingawa hayupo fit kwa asilimia 100.kinacho nishangaza ni kwa nini MARIO GOTZE amekubali kuikosa fainal hii wakati anasumbuliwa na tatizo la misuli tu!!!
                                                                    

Ilkay GUNDOGAN leo itabidi apande kwa juu ili akazibe nafasi ya MARIO GOTZE huku kwenye dimba akimuacha ama NURI SAHIN au GROSS kwa ajili ya kukumbana na kina SCHWEINSTIGER na MARTINEZ.Inaripotiwa kwamba mats hummels hayuko fit kwa hiyo atakuwa na kibarua kizito cha kumzuia MARIO MANDUZKIC mwenye nguvu na usumbufu pale mbele.
                                                                               


nadhani BVB watataka kushinda kwa kupitia kati,sehemu ambayo naiona itakuwa ngumu sana kwao.
anyway,atakayetumia makosa vizuri ya mwenzie ndiye atakaye ibuka mshindi.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!