Searching...
Image and video hosting by TinyPic
17 May 2013
Friday, May 17, 2013

INGIA HAPA KUMUONA EMMENUEL OKWI WA KINIGERIA.

 Huyu ni kijana wa kinigeria ambaye amekuja Tanzania kutafuta timu ya kuchezea tangu mwaka jana mwezi September anaitwa RAZAQ ADEMOLA.Kwa maelezo yake ana umri wa miaka 19.Ukiangalia hapa UTAGUNDUA KUWA watanzania tunaweza kujifunza kitu, hawa jamaa wa magharibi mwa afrika wamekuwa busy sana kutafuta mafanikio lakini sisi watanzania tumekuwa tukisubiri tufuatwe.

Lazima tujifunze kutumia fursa kama hizi hata kama unakipaji kama cha MESSI huwezi fanikiwa kama umejifungia tu ndani. Naomba vijana wenzangu tujitokeza kuonyesha vipaji vyetu na tuwe watu wa kupigana hadi dakika za mwisho.



 Tanzania tuna vijana wengi ambao wanacheza soka lakini wamejificha ndani.najitahidi kuwatafuta lakini bado wanaendelea kujificha.Huyu dogo katoka Nigeria hadi Tanzania lakini watoto wa kitanzania hawajawahifika hata  UGANDA au KENYA kujaribu bahati zao.mpira sio mchezo wa bahati lakini lazima utoke ndo watu wakuone.





0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!