Takribani nusu ya wapenda soka walikuwa hawaamini kama stars inaweza kwenda Brazil kwenye kundi ambalo MOROCCO na IVORY COAST wamo,kilichofanyika ni kuinga mkono tu timu ya nyumbani.
Nusu yao tayari wanaamini tunaweza shiriki CHAN na AFCON.sisi watanzania ni wepesi sana wa kukata tamaa na kuwakatisha wengine.Na hisi kama timu itashindwa kufuzu kwa michuano hii tena,yatatoka maneno ya dharau,kejeli na dhihaka kwa Stars pengine kuliko hata ambayo nimewahi yaskia.
Ninauhakika kuna watanzania wachache sana wanaojua sababu za stars kutofanya vizuri na njia ya kuzitatua,wengine ni kelele tu.Tunahitaji mjadala wa kitaifa ili wataalam watueleze tatizo ni lipi,na namna ya kulitatua vinginevyo,tutakuwa tunafanya operation ya kichwa kwa mgonjwa mwenye tatizo la mguu.
0 comments:
Post a Comment