Pigo kwa Manchester city,Aguero kuikosa As Roma.
Na Florence George
Mshambuliaji tegemeo wa Manchester City Muargentina Sergio Aguero ataikosa mechi ya ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya As Roma mchezo ambao unatarajiwa kuwa mkali huku kila timu ikiwa na nafasi ya kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo,mechi itakayochezwa huko Rome nchini Italia.
Mshambuliaji huyo aliumia kifundo cha mguu katika mechi ya ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya Everton ,mechi ambayo iliisha kwa Manchester City kushinda goli 1-0,goli lililofungwa na kiungo Mwafrika Yaya Toure kwa mkwaju wa penati.
Aguero ambaye hadi sasa ameshafunga magoli 19 katika mechi 19 alizocheza msimu huu atakosekana dhidi ya As Roma, mechi ambayo ni muhumu kwa pande zote mbili kwani timu zote zina nafasi ya kufuzu huku zikiwa na pointi tano kila moja huku wakiiombea CSKA Moscow ifungwe na Bayern Munich.
Taarifa za awali zinasema kuwa mshambuliaji huyo atakosekana uwanjani takribani mwezi mmoja, huku akitarajiwa kufanyiwa vipimo tena siku ya Jumatatu au Jumanne.
Manchester City itashuka dimbani siku ya Jumatano Usiku huku wakiwa na wasiwasi na baadhi ya wachezaji wake muhimu kama watakuwa fiti asilimia zote kuwavaa wataliano hao,wachezaji hao ni nahodha Vicent Kompany,David Silva,Jovetic ,Edin Dzeko huku Yaya Toure akitumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata walipocheza na CSKA Moscow.

0 comments:
Post a Comment