Searching...
Image and video hosting by TinyPic
17 May 2013
Friday, May 17, 2013

KUNG"ATUKA KWA FERGUSON

mzee huyu ni moja kati ya nembo kubwa sana katika medani ya soka kwenye EPL na Dunia.kila kitu kina mwanzo na mwisho,amefanya makubwa na kafanya vizuri kupumzika.Maana kadri anavyozidi kuzeeka,amekuwa akifanya ufundi mpaka anapitiliza.

Mzee Fergie anaipenda sana united na kwa umri wake kukutana na mazingira kama yale ya kukosa ubingwa msimu uliopita sekunde ya mwisho,namna alivyotolewa na Madrid msimu huu na aina ya kipigo alichopata toka kwa Barca fainal ya UCL hadi mikono ikatetemeka NI HATARI KWA AFYA YAKE.

Kwa namna Fergie anavyoipenda united,nadhani hato kubali man u ifungwe kirahisi bila kutia neno.anaweza akamnyima Kocha ajaye uhuru na kuanza kumuendesha kwa rimoti.

Fergie alifikia hatua ya kulingana jina na Club yake,yaani ukiita man u nisawa na kusema Ferguson na kinyume chake.kiti alichokiacha ni cha moto na sio kila mtu anaweza kukalia.kocha anayetakiwa sio wakufanya tu united ishinde bali muonekano wa club,hadhi na nembo ya united kuendelea kutamba.

  wakati katangaza kuachia ngazi eti kila mtu anasikitika,"ooh! babu kang'atuka" "ooh we love you" acheni mambo yenu bwana,imetosha acha apumzike!!

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!