KOCHA WA YANGA KAANZA KUTOA SABABU KUELEKEA KUWAVAA MGAMBO
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young Africans kesho watashuka dimbani kucheza na timu ya Mgambo JKT kutoka mjini Handeni katika muendelezo wa michezo ya VPL 2013.14 kipute kitakachofanyika kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga.
Young Africans ambayo iliwasili jana mchana jijini Tanga na kufanya mazoezi katika viwanja vya shule ya sekondari Galanos jioni kabla ya leo timu kufanya mazoezi asubuhi katika dimba la mkwakwani ambapo pia washabiki walijitokeza kwa wingi kuiona timu hyo yenye wachezaji wenye kiwango cha hali ya juu.
Kocha Mkuu wa Young Africans mholanzi Hans Van der Pluijm amesema anashukuru timu ilifika salama jijini Tanga na vijana wake wote kuweza kufanya mazoezi kwa siku mbili pasipo kuwa na majeruhi wala mchezaji mwenye tatizo lolote.
"Uwanja wa Mkwakwani sio mzuri hasa kwenye sehemu ya kuchezea kutokana na kuwa na mashimo mashimo hivyo mara nyingi mipira hudunda na kuwapita wachezaji, tumeliona hilo na kuwaeleza vijana wawe makini naamini kesho wakicheza na Mgambo watakua makini na kutumia nafasi watakazozipata kuweza kuibuka na ushindi" alisema Hans.
Mchezo wa kesho ni muhimu kwa Young Africans kuweza kuibuka na ushindi kwani pointi 3 katika mchezo huo, zitawafanya watoto Jangwani kufikisha alama 49 na kuwa na tofauti ya pinti 1 dhidi ya Azam FC wanaongoza ligi.
Wapenzi, wanachama na washabiki wa Young Africans manombwa kujitokeza kwa wingi kesho Uwanja wa Mkwakwani kuja kuwapa sapoti vijana katika mchezo huo muhimu.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa website ya YANGA.
0 comments:
Post a Comment