Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 December 2014
Thursday, December 04, 2014

Alan Pardew wa Newcastle aitikisa Chelsea.


Na Oscar Oscar Jr

Kocha mkuu wa Newcastle United, Alam Pardew ameibuka na kudai kuwa, pamoja na ubora walikuwanao Chelsea, haiwezekana wakacheza mechi zote msimu huu bila kufungwa. 

Pardew amesema hii ni timu imara ambayo hajawahi kuiona huku akisema kuwa ameanza kuitazama Chelsea tangu akiwa na mika 12 na bila shaka Mourinho atakuwa akijivunia.

Kocha huyo amesisitiza kuwa, bado Chelsea ni timu inayofungika lakini hakusita kusema kuwa wako kwenye kiwango kizuri kwa sasa. 

Newcastle United watawakaribisha Chelsea kwenye dimba la St. Jame's Park Jumamosi hii kwenye mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza.

Chelsea bado ndiyo vinara wa ligi hiyo huku wakiwa na alama 36 na wakiwa kama timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote wa ligi kuu msimu huu. 

Wataingia kwenye mchezo huo bila ya moja ya wachezaji wake bora msimu huu, Nemanja Matic baada ya kiungo huyo kupata kadi ya njano kwenye mchezo wao dhidi ya Tottenham Hotspurs na kuwa kadi yake ya tano msimu.

Nahodha wa Newcastle United, Fabricio Coloccini ambaye ulikosekana kwenye michezo mingi mwezi Novemba, anatarajia kurejea na kama vipimo vitatoa majibu mazuri anaweza kutumika kwenye mchezo huo. 

Newcastle United kwa sasa, wanapointi 20 huku wakishika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi kuu. Chelsea wametoka kupata Ushindi wa bao 3-0 dhdi ya Tottenham huku Newcastle United, wao wakitoka sare ya 1-1 na Burnley mechi iliyopita.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!