Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 December 2014
Monday, December 01, 2014

Klopp bado yupo yupo sana.


Na Chikoti Cico.

Kocha wa Borrusia Dortmund, Jurgen Klopp amesisitiza bado hajafikiria kuachia ngazi kwenye timu hiyo ingawa kwasasa Dortmund inashika mkia kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga ikiwa na alama 11 baada ya michezo 13 toka kuanza kwa ligi hiyo.

Timu ya Dortmund ambayo ilimaliza msimu uliopita wa ligi ya Bundesliga ikiwa nafasi ya pili nyuma ya Bayern Munich na wamekuwa na matokeo mabovu toka kuanza kwa msimu wa 2014/15 hasa kwenye ligi ya Bundesliga.

Toka kuanza kwa msimu huu wa Bundesliga mpaka sasa Dortmund wamecheza michezo 13 na kushinda michezo mitau, kutoka sare michezo miwili na kufungwa michezo nane huku wakipitwa na vinara wa ligi hiyo timu ya Bayern munich kwa tofauti ya alama 22 matokeo ambayo yanaiweka hatarini kazi ya kocha wa timu hiyo Jurgen Klopp.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya mchezo dhidi ya Eintracht Frankfurt ulioisha kwa Dortmund kufungwa kwa magoli 2-0,  kocha huyo alisema “Ninawajibika kadri ya uwezo wangu kwa sababu hakuna mtu ambaye amekuja na kusema kuwa anaweza kuifanya vyema kazi ya kufundisha kuliko mimi hivyo siwezi kuondoka”

“Kadri ambavyo hakuna suluhisho zuri basi siwezi kuondoka, wajibu ninaojiksia ni mzuri, kama ni kwamba bahati yetu imekwisha na kocha mpya ataweza kurejesha bahati nzuri basi mpigie na unihakikishie halafu ntaondoka lakini siyo rahisi”

Pamoja na matokeo hayo mabovu kwenye ligi ya Bundesliga, Dortmund wamefanikiwa kuvuka hatua ya makundi kwenye ligi ya mabingwa Ulaya huku mpaka sasa wakiongoza kundi D wakiwa na alama 12 baada ya michezo mitano.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!